Mwanasiasa
mkongwe ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya uchumi nchini Profesa
Ibrahimu Lipumba amesema anaunga Mkono Mpango wa serikali wa Miaka
mitano huku akisema ni vema Serikali ihakikishe inawekeza zaidi katika Nishati ya umeme ili kufikia lengo la kuwa nchi ya viwanda.
Wakati Tayari Mpango wa Serikali
ukiwa Umekwishawasilishwa kwa Miaka Mitano ijayo, ambapo Umeanisha namna
utakavyofanikisha Asilimia 40 ya Ajira ifikapo mwaka 2020 Zikitokana na Viwanda, huku Miongoni mwa Miradi Mikubwa uinayotarajiwa kutekelezwa ya Viwanda ni ujenzi wa kiwanda cha chuma.
Aidha Mchumi huyo pia amesema
adhima ya serikali ya kujenga nchi Ya Viwanda itafanikia ikiwa itawekeza
katika nishati ya Umeme wa Uhakika, licha Ya miradi mikubwa kama ya
Power Afrika na MCC kusitishwa huku akiishauri Serikali kufanyia kazi Maazimio ya bunge kuhusu sakata la Tegeta esrow.
Mahojiano hayo Maalum yamefanyika
Dar es Salaam, muda mfupi Baada ya Prof Lipumba kupokea Ujumbe maalum wa
wawafuasi wa chama cha CUF kutoka mjini Bagamoyo waliokuwa lengo la
msihi kurejea kwenye nafasi yake Ya Uenyekiti wa chama cha CUF.
No comments:
Post a Comment