Katibu Mkuu: Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi
Joseph Nyamhanga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanza
kutozwa kwa vyombo vya usafiri vitavyopita katika Daraja la Nyerere
kuanzia jumamosi ya Mei 14.
Na Kalonga Kasati
Serikali
imetangaza rasmi kuanza kwa tozo kwa vyombo vya usafiri vitakavyopita
katika daraja la Nyerere kuanzia Jumamosi tarehe 14 ,mwezi huu.
Akizungumzia na
waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema kuwa
kuanzia siku hiyo , vyombo vyote vya usafiri vitatakiwa kulipia
ushuru wa kupita katika daraja la Nyerere.
“ Tumeanza kutoza
tozo hii mara baada ya kufunguliwa kwa daraja hili na kuanza kutumika
kwa kupita bila kulipa kwa vyombo vya usafiri tangu Aprili 19 mwaka huu
na sasa tunaanza rasmi kutoza tozo kwa ajili ya kukusanya gharama za
usimamizi, utunzaji na uendeshaji wa daraja hili.” alisema Mhandisi
Nyamhanga.
Mhandisi
Nyamhanga amefafanua kwamba watembea kwa miguu watapita bure katika
daraja hilo huku wenye baiskeli wakilipia Sh. 300, pikipiki Sh. 600,
waendesha maguta ,bajaji na magari ya kawaida(Saloon Cars) watatakiwa
kulipia Sh.1500.
Mabasi yanayobeba
abiria 15 yatalipia Sh. 3,000, yale ya abiria zaidi ya 15 Sh. 5,000
na yale yanayobeba abiria zaidi ya 29 yatalipia Sh. 7,000.
Aidha magari
yenye tani zaidi ya mbili mpaka saba yatalipia Sh. 7,000, tani 7 hadi 15
watalipa Sh.10,000, tani 15 mpaka 20 watalipa Sh.15,000 na yale yenye
tani 20 mpaka 30 yatalipia Sh. 20,000.
Mhandisi
Nyamhanga ameongeza kuwa magari yenye namba za Jeshi la Wananchi(JWTZ),
Jeshi la Polisi(PT), Jeshi la Magereza(MT), gari za wagonjwa, magari ya
zimamoto na magari yenye vibali maalum yataruhusiwa kupita bure.
No comments:
Post a Comment