Mgombea urais anayeongoza katika
kinyang’anyiro cha kumteua mgombea wa chama cha Democratic Hillary
Clinton amekataa kushiriki mdahalo wan ne dhidi ya mpinzani wake Bernie
Sanders.
Bi Clinton alikuwa awali amekubali kushiriki mdahalo wa mwisho kabla ya mchujo muhimu katika jimbo la California na katika majimbo mengine matano wiki mbili zijazo.
Bw Sanders, Seneta wa Vermont, amesema hajashangazwa na uamuzi huo wa mpinzani wake.
Na katika hatua inayoonesha viongozi wa Democratic hawataki kumtenga Bw Sanders na wafuasi wake, wametangaza kwamba mgombea huyo ataruhusiwa kuteua theluthi moja ya kamati ya kuandaa ajenda ya mkutano mkuu wa chama cha Democratic mwezi Julai.
Mkutano huo hutumiwa kuidhinisha mgombea urais wa chama cha Democratic.
Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika mwezi Novemba.
No comments:
Post a Comment