Monday, 16 May 2016

Arsenal Wenger Arsenal: Kuingia katika soko la biashara ya wachezaji rasmi

 
Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameahidi kutumia pesa kadri itakavyohitajika katika kipindi cha dirisha la usajilia mbacho kitaanza rasmi mwezi ujao.

Wenger ameahidi kufanya hivyo, alipohojiwa na shirika la utangazi la Uingereza (BBC), Ambapo amesisitiza kwamba mfanyabiashara kutoka nchini Marekani mwenye hisa nyingi kwenye klabu ya Arsenal, Stan Kroenke amemuhakikishia suala hilo.

Wenger, amesema umefika wakati wa kuiona Arsenal inangia katika soko la biashara ya wachezaji pasi na kuhofia uwepo wa klabu nyingine ambazo zimekua zikitumia fedha nyingi Bila kujali thamani ya mchezaji.

Mzee huyo kutoka nchini Ufaransa, amekiri kuwa katika mipango ya kuwafuatilia baadhi ya Wachezaji ambao ameridhishwa na uwezo wao wa kucheza soka, na ameahidi kuanza kufanya kweli katika usajili wakati wowote mara baada ya msimu wa 2015-16 kufikia kikomo hapo jana.

“Nitafanya usajili wa mchezaji yoyote nitakaeona ananifaa, nimehakikishiwa kuwa uhuru wa kusajili popote pale, hivyo ninawatoa shaka mashabiki wa Arsenal.” Alisema mzee huyo Mwenye umri wa miaka 66.

Katika hatua nyingine, Wenger, amekanusha taarifa za kuwa mbioni kusaini mkataba mpya na klabu ya Arsenal, kama ilivyoripotiwa mwishoni mwa juma lililopita.

“Ninaamini kila jambo lina wakati wake, lakini hakuna chochote kinachoendelea kati yangu na Uongozi kuhusu suala la kusaini mkataba mpya,”

“Tunapaswa kuwa wastahamilivu na kuona nini kilichopo katika mwaka mmoja uliosalia katika mkataba wangu, lakini kwa hayo mengine yanayozungumzwa kuhusu mkataba mpya Sifahamu chochote.” Aliongeza wenger

No comments:

Post a Comment