Watu
wanne wamekufa papo hapo na wengine 29 kujeruhiwa baada ya basi la HBS
linalodaiwa kuwa ni Mali ya kampuni ya Sabena Walilokuwa Wakisafiria
kutoka Jijini Mbeya kwenda Tabora kuacha njia na kupinduka katika eneo
la Maji mazuri, barabara kuu ya Mbeya – Chunya wilayani Mbeya.
Basi hilo likiwa limebeba abiria Wengi kuliko uwezo wake, lilianza Safari Yake ya kuelekea Tabora likitokea jijini Mbeya, lakini inadaiwa
kuwa likiwa kwenye Mtelemko na kona kali za Mlima Mbeya likafeli breki
na ndipo Dereva Wake akaamua kuruka na kuliacha likijiendesha lenyewe
hali Ambayo ilisababisha lipoteze Mwelekeo na kuanguka mtaroni.
Muuguzi
wa Zamu katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya nyanda za Juu kusini,
Jesca Kahangwa amethibitisha kupokea miili ya watu wanne na Majeruhi 29
wa ajali hiyo, Huku akidai kuwa hali za Majeruhi Wengi Bado ni Mbaya.
Mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mbeya, Amos Makalla amewahi
katika eneo la ajali na baada ya kupata maelezo ya chanzo Cha ajali
hiyo, akaliagiza jeshi la polisi kuwatafuta na kuwakamata haraka Dereva,
kondakta na mmiliki wa Gari hilo kwa kosa la kuendesha Gari bovu Barabarani.