Tuesday, 30 May 2017

Ernesto Valverde kocha mpya Barcelona

Ernesto Valverde
Klabu ya Barcelona imemtanga rasmi kocha wa zamani wa Athletic Bilbao Ernesto Valverde kuwa kocha wao mkuu mpya
Valverde ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Barcelona,wiki iliyopita  alitangaza kuwa anaondoka Athletic baada ya kudumu klabuni hapo kwa takriban miaka minne.
Meneja huyo, mwenye umri wa miaka 53, atamrithi Luis Enrique, ambaye alitangaza tangu mwezi Machi mwaka huu kwamba anaondoka Barcelona baada ya mkataba wake wa miaka mitatu kumalizika.

Kufuatia Ghasia zinazoendelea Sudan kusini, Wanawake wakimbia makazi


wanawake na Watoto wazidi kuikimbia Sudan kusini
Maelfu ya wanawake na watoto kutoka Sudan kusini wamevuka mpaka kuingia nchini Sudan tangu kuanza kwa mwaka huu, wakikimbia ghasia na kitisho cha njaa.
Kwa mujibu wa Shirika la Kuwahudumia Wakimbizi Duniani -UNHCR- Karibu Wasudan kusini laki moja na 37 elfu wameingia nchini Sudan tangu Januari mosi, huku wengine zaidi ya laki moja na 31 elfu wakiwa tayari wamewasili nchini humo tangu mwaka 2016.
Wafanyakazi wa misaada wanaarifu kuwa wengi ya watu hao wanaowasili sasa ni wanawake na watoto.
Mkurugenzi wa Shirika la Msalaba mwekundu, kanda ya Afrika Dokta Faroumata Nafo-Traore wengi wanakuwa wamedhoofika kiafya na wamekuwa na msongo wa mawazo kutokana na hali iliyowatokea huko wanakotoka.

Kanisa la Maombezi GRC wamtembelea Spika wa Bunge

unnamed
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mchungaji Anthony Lusekelo (kulia) alipomtembelea leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
1
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akipiga picha ya pamoja na ugeni kutoka Kanisa la Maombezi (GRC) ukiongozwa na Mchungaji Anthony Lusekelo (wa tatu kulia) baada ya kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
2
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza jambo wakati alipotembelewa na ugeni kutoka Kanisa la Maombezi (GRC) ulioongozwa na Mchungaji Anthony Lusekelo (wa pili kulia) katika kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
A
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kulia) akimsikiliza Mchungaji Anthony Lusekelo (kulia) kutoka Kanisa la Maombezi (GRC) pale alipomtembelea leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.

Mzee Aliyechora Nembo ya Taifa afariki Dunia katika Hospitali ya Muhimbili



Monday, 29 May 2017

ZILIZOTANDA VICHWA VYA HABARI KATIKA KURASA ZA MBELE MAGAZETINI LEO JUMANNE MEI 30 2017




Mangu:Sirro Mchapakazi mzuri

Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu amewataka wananchi kumpa ushirikiano IGP mpya, Simon Sirro katika kukabiliana na matukio ya uhalifu nchini hasa katika Mkoa wa Pwani.
Mangu ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya Rais John Magufuli kumwapisha Sirro kuongoza jeshi la polisi nchini.
Mangu ambaye anasubiri kupangiwa kazi nyingine amesema anamfahamu Sirro kama mchapakazi mzuri na ataweza kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa na amani.
Alipoulizwa wito wake kwa Sirro kuhusiana na hali tete katika wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani, Mangu amesema "Sirro anafahamu anachotakiwa kufanya katika hilo, nimefanya naye kazi kwa karibu, ninachoomba ni askari na wananchi wote wampe ushirikiano."
Sirro ameapishwa leo kuwa IGP, kabla ya uteuzi huo alikuwa kamanda wa polisi (RPC) katika mikoa ya Tanga, Mwanza na Shinyanga. Baadaye alikwenda kitengo cha operesheni na mafunzo polisi makao makuu, kisha akahamishiwa kitengo hicho kanda maalumu ya Dar es Salaam kabla ya kuwa kamishna wa kanda hiyo.

Nape:Kimsingi kazi kubwa ya Mbunge hasa wabunge wa CCM ni kuishauri serikali yake

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amefunguka na kusema wabunge wa Chama Cha Mapinduzi ambao wanaishauri na kuikosoa serikali ni watu ambao wana mapenzi mema na Rais na serikali yake kuliko wanao sifia kila kitu.
Nape Nnauye amedai wabunge ambao kazi yao ni kusifia kila kitu hata kama kuna mapungufu hao hawana mapenzi ya kweli kwa Rais Magufuli na serikali kiujumla na kudai yeye anaitumia nafasi yake vizuri kutoa ushauri kwa serikali kupitia bunge sababu ndiyo njia sahihi aliyonayo kwa sasa.
"Kimsingi kazi kubwa ya Mbunge hasa wabunge wa CCM ni kuishauri serikali yake sisi tunaoshauri tunampenda zaidi Rais na tunaipenda zaidi serikali ifanye vizuri kuliko wale ambao watakuja na kusifu na kupongeza kwa kila kitu, hata pale wanaona kabisa hapa tungeweza kushauri na mambo yakarekebishika" alisema Nape Nnauye
Mbali na hilo Nape Nnauye amedai kuwa watu ambao wanashangaa yeye kuishauri serikali sasa kupitia bunge anasema hawafahamu pia alipokuwa kwenye Baraza la Mawaziri, alikuwa akifanya hivyo.

Taifa Stars yatarajia kuweka kambi Misri

Kikosi cha wachezaji 20 wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania 'Taifa Stars' kinatarajiwa kuondoka kesho Jumanne saa 10.45 jioni kwenda Misri kufanya kambi ya siku nane kujindaa na mchezo dhidi ya Lesotho utakaofanyika Juni 10, 2017, Dar es Salaam.
Wachezaji hao 20 kutoka hapa Tanzania wataungana na wengine watatu ambao ni Nahodha Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Faridi Mussa wanaocheza ughaibuni katika kikosi hicho na kufanya jumla ya wachezaji kuwa 23 nchini Misri.
Nahodha Msaidizi, Jonas Mkude hatakuwepo kwenye msafara huo kutokana na ushauri wa madaktari walioelekeza kwamba nyota huyo wa Simba apate mapumziko ya angalau siku nne.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga ameridhia na kusema kuwa Mkude ataungana na wenzake Juni 8, mwaka huu timu itakaporejea kutoka Misri. Mayanga hajajaza nafasi ya Mkude.
Mchezo dhidi ya Lesotho ni muhimu kwa Tanzania ikiwa ni mechi ya kwanza kwa Taifa Stars katika Kundi 'L' kuwania nafasi muhimu ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2019 zitakazofanyika NCHINI Cameroon.
Mbali ya Lesotho na Tanzania, mataifa mengine katika Kundi 'L' ni Uganda na Cape Verde ambao pia wikiendi ya Juni 9, 10 na 11, mwaka huu watakuwa katika mchezo wa kwanza pia kuwania nafasi hiyo.
Kikosi cha Taifa Stars kinaundwa na makipa Aishi Manula  (Azam FC), Benno Kakolanya  (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
Walinzi wa pembeni upande wa kulia ni Shomari Kapombe    (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Haji Mwinyi  (Yanga SC).
Walinzi wa kati Erasto Nyoni  (Azam FC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Agrey Morris  (Azam FC) ilihali viungo wa kuzuia ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude kutoka Simba SC ambaye hatasafiri na timu kwa sasa.

Tuzo ya Mchezaji Bora Wa Mwaka Chelsea, Kante

 Bao la msimu: Eden Hazard
Mchezaji wa mwaka wa wachezaji: N'Golo Kante
Mchezaji wa mwaka (wanawake): Karen Carney
Mchezaji bora wa Akademi: Mason Mount
Mchezaji bora wa mwaka: Eden Hazard
Utambuzi maalum kwa kazi bora: John Terry





Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima

unnamed
 Mtaalam wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima Bw. David Plotner (kushoto) kutoka shirika la CDC Marekani akijadiliana na maafisa wa TEHAMA wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Munir Mdee (katikati) na Abdullah Othman (kulia) wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
 1
Afisa TEHAMA kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Munir Mdee akitoa mafunzo ya kutumia Dodoso kwa njia ya tablet kwa washiriki wa mafunzo ya Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
 2
  Mratibu wa  Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima Bi. Hellen Hillary (kushoto) kwa upande wa Tanzania Bara akijadiliana na mratibu wa utafiti huo kwa upande wa Tanzania Zanziar  Bi. Nuru  Masoud (kulia) wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
 3
 Meneja wa Takwimu za Jamii Bi. Sylvia Meku (katikati) akiwaelekeza washiriki wa mafunzo ya awali ya Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima Bw. Frank Mapendo (kushoto) na Jocelyne Rwehumbiza (kulia) wakati wa mafunzo ya awali ya utafiti huo yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unatarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
 4
 Mwananchi kutoka kata ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam akijibu maswali kutoka kwa Mtakwimu Bw. Stephen G. Cosmas wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakati wa majaribio ya Dodoso litakalotumika wakati wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unaotarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.
 5
 Mtakwimu Bi. Hellen Mtove wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu akimhoji mwananchi kutoka kata ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam wakati wa majaribio ya Dodoso litakalotumika wakati wa Utafiti wa Matumizi ya Tumbaku kwa Watu wazima unaotarajia kufanyika nchini mwezi Agosti, 2017.(PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

Hafla ya kuapishwa IGP Simon Sirro Ikulu jijini Dar es Salaam

unnamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimvalisha vyeo vipya Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro kabla ya kumuapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.
1
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro akila kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro akila kiapo cha uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro akisaini Hati ya Kiapo cha Uadilifu Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro mara baada ya kula kiapo Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba,IGP mpya Simon Sirro,  IGP wa zamani Ernest Mangu pamoja na viongozi mbalimbali wa Jeshi la Polisi pamoja na Magereza.
1
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Inspekta Jenerali wa Polisi(IGP) Simon Sirro pamoja na IGP wa zamani Ernest Mangu Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na IGP wa zamani Ernest Mangu Ikulu jijini Dar es Salaam.
2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Majeshi ya Polisi na Jeshi la Wananchi  mara baada ya kumuapisha IGP Simon Sirro Ikulu jijini Dar es Salaam.
unnamed
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba mara baada ya tukio la uapisho wa IGP Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU

Mgogoro wa maduka Arusha Madiwani wahusika


Na Mwandishi Wetu, Arusha 
Mkurugenzi
wa Jiji la Arusha Bw Athuman Kihamia amekataa kamati ya watu 4 mbele ya
Baraza la madiwani wa Jiji la Arusha iliyokuwa imepangwa kwa ajili ya
kuchunguza mgogoro wa maduka hayo 396 yalipo stand ndogo Jiji la Arusha
kwa kile alichosema kuwa wananchi bado wanawatuhumu madiwani wengi kuwa
chanza cha migogoro hiyo.
 
Mkurugenzi
huyo amesema kuwa binafsi haoni sababu za msingi za uwepo wa kamati hiyo
badala yake ana hofu ya kuingizwa siasa katika jambo hilo.
 
Kuhusu
wajenzi wa vibanda vya maduka stand ndogo,  mkurugenzi wa jiji la
Arusha Bw Athumani Kihamia amewataka madiwani kutokuweka maneno ya
kisiasa katika swala hilo la kimaendeleo ambapo mpaka sasa mgogoro wa
maduka hayo takribani 396 upo katika mahakama ya ardhi jiji la Arusha.
 
Aidha
pia mkurugenzi wa jiji la Arusha ameongeza kwa kusema kuwa mapato
makubwa ya jiji la Arusha yalikuwa yanakusanywa kupitia maduka hayo
takribani 1196 hapa jijini maduka hayo ambayo yapo maene ya Stand
ndogo,Soko kuu,Kilombero na kijenge ambapo halmashauri ilikuwa
inakusanya shilingi Bilioni 1.2 kwa mwaka kitu ambacho kwasasa ameeleza
kuwa mapato hayo yanaweeza kupungua kutoka na mgogoro wa maduka 396
yalipo maeneo ya Stand ndogo jijini Arusha na kubaki maduka 800 yanayo
tegemewa na halmashauri hiyo ya jiji la Arusha
 

Ummy Mwalimu:Hakuna mgonjwa yeyote aliyehisiwa au kuthibitishwa kuwa na virusi vya Ebola hapa nchini

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kufuatia kupatikana kwa taarifa ya ugonjwa wa Ebola huko DRC Congo hakuna mgonjwa yeyote aliyehisiwa au kuthibitishwa kuwa na virusi vya Ebola hapa nchini hadi wakati huu.
Akizungumza na vyombo vya habari leo, Mwalimu alisema nchi yetu inapakana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hata hivyo kuna uwezekano wa ugonjwa huo kuingia hapa nchini kutokana na mwingiliano  wa watu, hasa wasafiri wanaotoka na kuingia.
Alisema kutokana na hali hiyo wizara inaendelea kuchukua tahadhari ili kuzuia ugonjwa huu usiingie hapa nchini.
"Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu, waendelee kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huu.  Aidha Wizara inaendelea kusisitiza kuwa hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa huu hapa nchini," alisema Ummy.

Sunday, 21 May 2017

ZILIZOTAWALA MAGAZETINI LEO MEI 22 2017 JUMATATU




Gwajima:Sitokufa hadi nitakapotimiza lile lililomleta duniani

  Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema hatakufa hadi pale atakapotimiza lile lililomleta duniani.
 Ameyasema hayo leo wakati wa ibada ya Jumapili kanisani kwake ikiwa ni siku chache baada ya mhubiri mmoja wa kimataifa kutabiri kuwa Gwajima atakufa ifikapo 2018.
“Mungu ndiye anajua siku saa na dakika ya kufa kwangu si mwanadamu,” amesema Gwajima

Korea Kaskazini yafanya jaribio la kombora jingine

Jeshi la Korea Kusini linasema kuwa Korea Kaskazini imefanyia majaribio kombora lingine.
Ofisi ya kijeshi nchini Korea Kusini inasema kuwa kombora hilo lilirushwa siku ya Jumapili jioni saa za Korea.
Jaribio hilo linafanyika wiki moja baada ya Korea Kaskazini kulifanyia majaribio kombora lingine ambalo inadai kuwa ni jipya na ambalo lina uwezo wa kubeba silaha kubwa ya nuklia.
Jumatatu iliyopita baraza la usalama la Umoja wa Mataifa liliitaka Korea Kaskazinia kusitisha majaribio kama hayo.
Ulisisitiza umuhimu wa nchi hiyo kuachana na hatua hizo.
Korea Kaskania inafahamika kwa kuunda zana za nuklia na imefanya jumla ya jaribio matano ya nuklia na ya makombora yenye uwezo wa kosafirisha zana hizo hadi maeneo inayolenga.
Korea Kusini inasema kuwa jaribio la hivi punde lilifanyiwa eneo la Pukchang magharibi mwa nchi.

Rais Yoweri Museveni :Mimi ni zao la Mwalimu Nyerere

  Rais John Magufuli na Rais Yoweri Museveni wamesaini mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Ohima, Uganda hadi Tanga.
Akizungumza leo Ikulu wakati wa utiaji saini mkataba huo, Magufuli amesema walikuwepo matapeli wengi wakati wa mchakato wa ujenzi wa bomba hilo na kuwa anafurahia  zaidi kuingia mkataba huo na Uganda.

Timu ya Ruvu Shooting Yapata Ajali Mkoani Singida

Msafara wa Timu ya Ruvu Shooting Umepata Ajali mbele Kidogo ya Singida wakiwa safarini kurejea Dar es Salaam.
Ruvu Shooting walikuwa njiani wakiokea Shinyanga walipocheza mchezo wao wa kumalizia msimu wa 2016/2017 wa Ligi Kuu soka Tanzania bara dhidi ya Stand United
Taarifa kutoka kwa mmoja wa wachezaji waliokuwapo zinasema kwamba gari  hilo likiwa katika Mwendo, tairi lilipasuka na kusababisha gari kuhama Njia na kuparamia miti iliyokuwa jirani.
Hakuna mtu yoyote aliyeumia sana japo kuna mchezaji mmoja ambaye amepata Majeraha ya kawaida.


Mapokezi ya kombe la ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu 2016/2017.

Leo Mei 21, 2017 mashabiki wa Yanga walijitokeza kwa mamia kuipokea timu yao kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Dar wakati timu hiyo ikiwasili kutoka Mwanza ikiwa na kombe la ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu 2016/2017.