Monday 8 December 2014

Kocha Phiri apambanisha wachezaji Simba

Kocha Phiri apambanisha wachezaji Simba

 

 Wachezaji wa timu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam wakifanya mazoezi yao chini ya Kocha patrick Phiri, (hayupo pichani) wakijiandaa na mechi ya Mtani Jembe. Na Mpigapicha Wetu 



KOCHA Mkuu wa Simba, Mzambia Patrick Phiri, ameanzisha programu mpya ya mazoezi ambayo mara mbili kwa wiki itakuwa ikizikutanisha timu ya vijana ‘Simba B’ na ile ya wakubwa.
Kuhusiana na hilo, kocha huyo alisema: “Hili ni jambo jipya lakini litakuwa na faida kwa klabu ya Simba, timu ya vijana itaweza kujifunza na kupata uzoefu kutoka kwa wakubwa zao utakaowaanda kwa ligi.
Wakubwa nao watafaidika kucheza na vijana wenye damu changa kwani itawaongezea kasi na kuwafanya wawe bora zaidi kwenye Ligi Kuu.
“Wachezaji wa timu kubwa watatakiwa kuonyesha uwezo wa hali ya juu, anayeshindwa atashushwa hadi timu ya vijana,” alisema Phiri.
Baada ya Mchezo wa juzi Jumatano kati ya timu ya wakubwa na vijana, Phiri amempandisha kiungo mshambuliaji, Iddi Bahati.

No comments:

Post a Comment