Uongozi wa Yanga umesema hautaenda mahakamani kupinga Simba kupewa pointi tatu.
Simba imeshinda rufaa
yake dhidi ya Kagera Sugar na kupata pointi tatu na mabao matatu ikiwa
ni baada ya kubainika beki Mohamed Fakhi alicheza mechi dhidi ya Simba
akiwa na kadi tatu za njano.
Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amesema kama kuna wanachama wanataka
kwenda mahakamani, wao hawatakuwa na uwezo wa kuwazuia huku akisisitiza
Tanzania ikifungiwa, Serengeti Boys itang’olewa kushiriki michuano ya
Kombe la Mataifa Afrika na ile kauli mbio ya Gabon mpaka Kombe la Dunia
itageuka na kuwa “Gabon hadi Nyumbani Tanzania”.
“Wakiendelea hivi itakuwa ni Gabon hadi Nyumbani, haitakuwa Kombe la Dunia tena.
”Watu wana hasira
zao, sisi viongozi tunaweza tusijue kinachoendelea. Kagera ni timu
ndogo, wanaonewa, hawatendewi haki. Sasa sisi tumeinunua hii kesi.
“Ajabu kabisa,
waamuzi wameitwa wawili tu na wengine hawakuitwa. Hii si sawa, kuna
jambo hapa,” alihoji Mkemi akionekana ni mwenye jazba.
No comments:
Post a Comment