Wasafiri katika mji mkuu wa Uingereza London, hivi karibuni wataanza kutumia magari ya usafiri yasiyo na dereva.
Katika kipindi cha majuma matatu yanayokuja karibu watu 100 wataanza kutumia magari hayo katika eneo la Greenwwich mjini London.,
Magari hayo ambayo husafiri kwa hadi kasi ya kilomia 16.1 kwa saa, yataelekezwa na kompyuta.
Hata hivyo kutakuwa na mtu ndani ya gari hilo ambaye anaweze kulisimamisha ikiwa itahitajika.
Magari yasiyo na dereva kuanza kutumika London
Oxbotica, ambayo ni kampuni iliyounda magari hayo, ilisema kuwa watu 5000 wametuma maombi ya kutaka kushiriki katika majaribio hayo.
Magari hayo yanawabeba watu wanne na hayana usukani wala breki
Gari hilo lina kamera ambayo inaweza kuona umbali wa mita 100 na husimama wakati kuna kitu chochote mbele yake.
Maafisa wa mradi huo wanaamini kuwa magari hayo, yatasaidia katika kuboresha usafiri eneo la Greenwish jijini London.
No comments:
Post a Comment