Watu wengi nchini Argentina sio mara ya kwanza lakini wamezidi kumuona Messi kama msaliti anayewafanyia makusudi, wengi wanaona Messi hafurahii kuitumikia timu yake ya taifa kama ilivyo akiwa na Barcelona.
Sasa shemeji wa kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone aitwaye Carlos Dibos ameibuka na kumshambulia Messi hadharaninkwa kusema hafai kuichezea timu ya taifa na hajui thamani ya jezi ya Argentina.
Dibos ambaye alikuwa kocha wa viungo wa timu ya Argentina ameshawahi kufanya kazi na Messi mwaka 2006 na 2008 ameenda mbali zaidi na kusema Messi amekosa mvuto wa kuitwa mchezaji bora wa dunia.
“Sidhani kama mchezaji ni vibaya akachagua mtu wa kucheza naye au wa kumfundisha, lakini mchezaji huyo anatakiwa awe anajituma, jasiri,mfariji lakini pia awe tayari kuibeba timu katika mabega yake kama ilivyokuwa kwa Diego Maradona” alisema Dibos.
Kuhusu Lioneil Messi bado Dibos anaamini ni kati ya wachezaji bora duniani lakini haamini kama Messi ndio mchezaji namba moja dunia, na badala yake Dibos anaamini Neymar ni bora kuliko Lioneil Messi.
“Inabidi mchezaji awe anajua kuhusu jezi ya Argentina, kuvaa jezi hiyo unabeba matuamaini ya Waargentina wengine, kwangu mimi Maradona alikuwa mchezaji wa aina hiyo lakini kwa Messi hapana” aliongeza Dibos.
Dibos alimaliza kwa kusema “Messi ni kati ya wachezaji bora duniani lakini Neymar ni bora zaidi yake, tumechoshwa na hizi tabia hapa Argentina(tabia za Messi), na inabidi tuliweke hilo wazi”.
Messi amekuwa na wakati mbaya katika timu ya taifa kwani mara kadhaa ameshatishia kujiondoa katika timu hiyo, huku adhabu aliyopewa ikiiweka kwenye hatihati Argentina ya kukosa kushiriki kombe la dunia mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment