Friday, 14 April 2017

Mwandishi wa Habari Josephat Isango amefariki Dunia leo asubuhi

Isango.png

Taarifa za kustusha zimetufia asubuhi hii kuwa Mwandishi  Kijana mahiri wa Habari hapa Nchini Josephat Isango kuwa amefariki dunia,
taarifa hizo zinasema kuwa Isango amefariki Dunia katika Hospital ya Puma mkoani Singida alipokuwa amelazwa kwa muda kidogo tangu alipokuwa akisumbuliwa.
taarifa hizi zimethibitishwa na nduguye wa karibu aitwaye Christopher aliyekuwa akimuuguza.
Christopher amezungumza na Mhariri wa gazeti la MwanaHALISI Jabir Idrissa na kusema Isango amefia hospitalini Ikungi mkoani Singida.
Isango alilazwa hospitalini hapo kwa wiki mbili sasa akisumbuliwa na kifua. Hata hivyo uchunguzi wa afya yake ulibaini ana tatizo kwenye moyo.
Aliwahi kuugua akiwa jijini Dar es Salaam na baada ya muda mfupi aliamua kusafiri kwenda Singida, mkoa wa nyumbani kwao.
Isango amekuwa mwandishi wa habari maarufu kutokana kuhusika na matukio ya kuvutana na polisi.
Mwaka 2015 alishambuliwa na polisi wa FFU eneo la mbele ya makao makuu ya Jeshi la Polisi katikati ya jijini Dar es Salaam alipokuwa na waandishi wengine wakisubiri kuwasili kwa viongozi wakuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo  (CHADEMA).
Viongozi wa Chadema waliitwa na Jeshi hilo kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na tuhuma za kuchafua amani.
Kwa karibu miaka miwili, Isango alifanyakazi kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd  (HHPL) inayomiliki na kuchapisha gazeti la MwanaHALISI na kuendesha mitandao ya kinamii.
Alihamia akitoka kampuni ya Free Media inayomiliki na kuchapisha gazeti la Tanzania Daima. Lakini alipata kuandika habari na makala MwanaHALISI kwa njia ya kujitegemea tangu mwaka 2008.



Isango, mzaliwa wa kijiji cha Kisasida, mkoani Singida,  alisomea uandishi wa habari Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine Nyegezi jijini Mwanza.
Alikuwa mmoja wa waandishi wenye ujasiri wa kukabiliana na mazingira magumu ya kazi.
Alipoamua kuhama MwanaHALISI mhariri wake alisema itamchukua muda mrefu kupata mwandishi kijana mkakamavu kama Isango.



[​IMG]

No comments:

Post a Comment