Muda wa tangazo la hali ya hatari waongezwa Uturuki
Rais Recep Tayyip Erdogan atangaza muda zaidi wa hali ya hatari
Serikali ya Uturuki imesema kuwa imeongeza ukomo wa ongeza tangazo la
hali ya hatari nchini humo kwa miezi mingine mitatu.Hali ya hatari
nchini humo awali ilitangazwa kutokana na jaribio la mapinduzi mwezi
July,ambapo tangazo hili la sasa limekuja siku moja tu baada ya rais wa
taifa hilo Recep Tayyip Erdogan kupata ushindi mwembamba katika hatua
yake ya kutaka kuongeza muda wake madarakani.
Mapema Erdogan alisema kuwa atapuuza ukosoaji wa kimataifa katika kura
ya maoni iliyofanyika siku ya jumapili,akizungumza na waangaliazi wa
kimtaifa alisema kuwa wanapaswa kufahamu nafasi yake.Amesisitiza kuwa
angelishikilia kura ya maoni kwa zaidi ya muongo mmoja wa mazungumzo
kuhusiana na kujiunga na jumuiya ya Ulaya.
Hata hivyo maandamano yalianza mara tu baada ya upigaji kura huo.Murat
Kazanci ni muandamanaji kutoka mjini Istanbul anasema matokeo ni ya
uongo
"Na amini kulikuwa na mchezo mchafu na matukio mengi ya ukiukaji wa
sheria.Tulisikia habari nyingi.Tulisimama kidete kwaajili ya kura yetu
siku ile,hatukubaliani na kura ya ndiyo kwa sababu matokeo ilikuwa ni
kura ya hapana.
Haya ndiyo matokeo ya maandamano haya,anasema Bi. Yasar Bodur na kusisitiza kwamba kwanini anaandamana
Hapo jana rais wa sasa wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametangazwa kuwa
mshindi kwa asilimia 51 katika kura ya maoni iliyopigwa nchini
humo,ushindi unaotajwa kuwa ni mdogo baada ya kupata kiwango kidogo na
kwamba Erdogan mwenyewe hakutegemea matokeo hayo.

No comments:
Post a Comment