Thursday, 13 April 2017

Mshukiwa wa shambulio la Borussia Dortmund akamatwa

Maafisa wa polisi nchini UJerumani wanamshikilia mshukiwa mmoja anayehusishwa na itikadi kali za kiislamu kufuatia shambulio la bomu katika basi la timu ya Borussia Dortmund.
Viongozi wa mashitaka pia wamesema kuwa vilipuzi vitatu vilikuwa vipande vya chuma.
Maafisa wa polisi nchini Ujerumani wanachunguza uwezekano wa uhusiano wa kigaidi katika shambulio hilo , vyombo vya habari vya Ujerumani vimesema.
Barua iliopatikana katika eneo la tukio inataja shambulio la krisimasi la mjini Berlin pamoja na operesheni za kijeshi nchini Syria.
Haijabainika iwapo barua hiyo ilikuwa halisi.
Wakati huohuo viongozi wa mashtaka nchini Ujerumani ambao huongoza uchunguzi unaohusishwa na ugaidi wanaongoza uchunguzi huo.
Gazeti la Ujerumani la Sueddeutsch Zeitung lilisema kuwa barua hiyo inayoanza kwa ”Jina la mwenyezi mungu imesema Ujerumani inatumia ndege za Tornado katika muungano wa majeshi wanaopigana na Islamic State.
IS imesema kuwa ilitekeleza mashambulio katika soko moja wakati wa Krisimasi mjini Berlin.
Lakini kuna uwezekano washukiwa wanajaribu kuukanganya uchunguzi unaoendelea ,kulingana na gazeti hilo wakiongezea kwamba uchanganuzi wa barua hiyo unaofanywa na wataalam unaendelea.
Shirika la habari la Ujerumani DPA pia limeripoti kwamba kuna barua ya pili inayosambazwa katika mitandao ya kijamii ikidai kuwa kundi la mafashisti lilitekeleza shambulio hilo.

Barua ya pili ,ilichapisha maandishi ya kifashisti ikisema kuwa shambulio hilo linatokana hatua ya klabu hiyo kuwapendelea wafuasi wa mrengo wa kulia.

No comments:

Post a Comment