Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma
Serikali kupitia Mfuko wa
Maendeleo ya Vijana imetoa mikopo yenye thamani ya Shillingi Billioni
1.5 kwa vikundi vya vijana 129 katika Halmashauri mbalimbali nchini.
Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alipokuwa akitoa
hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya
mapato na matumizi ya fedha za Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.
“Serikali inaendelea na azma yake
ya kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi kwa kutoa mikopo yenye riba
nafuu”’ Alisisitiza Mhe. Majaliwa.
Aidha , Mamlaka za Serikali za
Mitaa kupitia mapato yake ya ndani zimetoa Shillingi Billioni 4.6 ikiwa
ni mikopo yenye masharti nafuu kwa vikundi vya vijana 2,356 na hatua
hizi zimekwenda sanjari na utengeji wa maeneo maalum yenye jumla ya
ekari 85,603 kwa ajili ya shughuli za vijana za Kilimo, biashara ndogo
ndogo, burudani na michezo.
Katika mwaka 2017/2018, Serikali
itaendelea kusimamia Halmashauri zote nchini kutenga asilmia 5 ya mapato
yao kwa ajili ya vijana na asilimia 5 kwa wanawake.
No comments:
Post a Comment