Sunday, 2 April 2017

Meli kubwa ya Korea Kusini yatoweka baharini

Meli kubwa ya Korea Kusini iliyokuwa na watu 24 imetoweka kusini bahari ya Atlantic.
Mabaharia wawili raia wa Ufilipino waliokolewa, kwa mujibu wa shirika la AFP.
Siku ya Ijumaa baharia mmoja alituma ujumbe uliosema kuwa meli hiyo yenye urefu wa mita 312, inayojulikana kama Stellar Daisy freighter, ilikuwa ikingia maji.
Jeshi la wanamaji la Uruguay lilijulisha meli zingine eneo hilo ambazo zilianza kuitafuta Msemaji mmoja wa jeshi naye alisema kuwa walihisi harufu kali ya mafuta.
Watu wawili waliookolewa walipatikatwa na meli za biashara zilizokuwa zikisaidia kutafuta meli hiyo.
Korea Kusini pia imeomba msaada wa kuitafuta kutoka Brazil na Uruguay.

Meli hiyo kubwa iliyo na uwezo kubeba tani 260,000 inayomilikiwa na kampuni ya Korea Kusini, ilikuwa na raia 16 wa Ufilipinona 8 wa Korea Kusini

No comments:

Post a Comment