Wiki hii kulikuwa na mchezo mjini Madrid kati ya Atletico na Leicester City, kama kawaida Leicester wakiwa na mashabiki wao wakorofi walikuwa mjini Madrid kuwakabili Atletico Madrid.
Ripoti zinasema muda mchache kabla ya mchezo huo kuanza ambao Leicester walifungwa bao 1, kulikuwa na kikundi cha mashabiki kama 70 waliokuwa wakileta fujo mjini hapo.
Wakati polisi walipojaribu kukabiliana na mashabiki hao ili kuwatuliza, mashabiki hao waliendelea na fujo na kupigana na polisi kiasi cha kuwajeruhi baadhi ya askari.
Hata hivyo baadhi ya mashabiki walikamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani,ambapo mahakama imeamua kuwahukumu kifungo cha miezi minane jela kutokana na kosa la kuleta fujo na kupigana na polisi.
No comments:
Post a Comment