Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Israel waje nchini kuwekeza
kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya kilimo.
Ametoa kauli leo (Jumatano, Aprili
5, 2017) alipokutana na Balozi wa Israel nchini Tanzania, Mheshimiwa
Yahel Vilan, Ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema Tanzania na
Israel ni nchini ambazo zina uhusiano mzuri kwa muda mrefu, ambapo
ameahidi kwamba Serikali itaendelea kuudumisha.
Pia Waziri Mkuu amewakaribisha
raia wa Israel kuitembelea Tanzania kama watalii kwa sababu kuna fursa
nyingi za utalii ukiwemo mlima wa Kilimanjaro na mbuga nyingi
zilizosheheni wanyama.
Kwa upande wake, Balozi Vilan
ameipongeza Serikali kwa utendaji wake, ambapo amesema viongozi wa
makampuni 50 kutoka nchini Israel wanatakuja nchini mwaka huu kushiriki
katika jukwaa la biashara na uchumi kati ya Tanzania na Israel.
Amesema mbali na kushiriki katika
jukwaa hilo, pia viongozi wa makampuni hayo watapata fursa ya kuangalia
maeneo mbalimbali ya uwekezaji nchini.
Pia Balozi Vilan amesema Serikali
ya Israel itaimarisha kitendo cha wagongwa mahututi (ICU) katika
hospitali ya Rufaa ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma pamoja na kuwajengea
uwezo watumishi wa kitengo hicho.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, APRILI 5, 2017.
No comments:
Post a Comment