Monday, 3 April 2017

The Guardian Limited yakanusha uzushi wa kufunga kampuni



Kampuni ya uchapishaji magazeti The Guardian Limited ambayo huchapisha magazeti ya The Guardian, Nipashe na Lete Raha, imekanusha taarifa za uzushi zilizosambaa mtandaoni kuwa inaifunga kutokana na ukata.
Taarifa hiyo ya uzushi ilisema:
Management ya The Guardian Chini ya General Manger, Ndg Srinivas imewatangazia wafanyakazi wa IPP- The Guardian kusudio la kufunga kampuni kutokana na ukata unaoikabili kampuni hiyo. The Guardian ni miongoni mwa kampuni kubwa za Magazeti wachapishaji wa Gazeti la kila siku la The Guardian, Nipashe, Lete Raha.
Wafanyakazi wa The Guardian wanaishi/Kupita katika kipindi kigumu hawajalipwa mshaara miezi 4 toka January 2017 wafanyakazi hawajalipwa mshahara. Frelencer na correspondence reporter hawajalipwa toka August 2016.
Media Solution (Wachapishaji wa Gazeti la Kulikoni na ThisDay) ambayo ni kampuni Dada wa The Guardian lilifungwa Rasmi mwezi February 2017. Wafanyakazi zaidi ya 200 wa Media Solution Ajira zao zilisitishwa mwezi uliopita. “Kimsingi hali ni Mbaya, kama Mzee Mengi anaisoma number inabidi tujitafakari kama Nchi tunaelekea wap?” Alinukuliwa mfanyakazi mmoja wa The Guardian akilalamika kwa uchungu.
Kufungwa kwa The Guardian kutasababisha wafanyakazi zaidi ya 350 kupoteza kazi.

No comments:

Post a Comment