Thursday, 13 April 2017

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imefanikiwa kukopesha bilioni 6.5 kwa Wakulima

ABO1
Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB.Hafla hiyo imefanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
ABO2
Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano (Kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia) wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB. Hafla hiyo imefanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
ABO3
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kushoto) akimuangalia Mkuu wa Huduma za Kisheria wa TADB, Bibi Neema Christina John (Katikati) wakati akiendelea na zoezi la ugongaji wa mihuri Mikataba ya Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.Mikataba hiyo ilisainiwa hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
ABO4
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kushoto) akimuangalia Mkuu wa Huduma za Kisheria wa TADB, Bibi Neema Christina John (Katikati) wakati akiendelea na zoezi la ugongaji wa mihuri Mikataba ya Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.Mikataba hiyo ilisainiwa hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
ABO5
Msajili wa Hazina Dk.Oswald Mashindano (Kushoto) akibadilishana Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia).Makubalizno hayo yamefanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
ABO6
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Aliyesimama) akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya makubaliano ya utekelezaji wa mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na TADB. Hafla hiyo imefanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam
ABO7
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (Katikati) akizungumza na Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano (Kulia). Anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kushoto). Hafla hiyo imefanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imefanikiwa kukopesha jumla ya shilingi bilioni 6.5 kwa vikundi 20 vyenye jumla ya wakulima 2575 ili kuisaidia Serikali katika kujenga Tanzania ya viwanda.
Hayo yamebainishwa leo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga wakati wa utiaji saini Mkataba wa Makubaliano ya Utekelezaji wa Mkakati wa mwaka kati ya Msajili wa Hazina na Benki hiyo katika hafla iliyofanyika Ofini kwa Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam.
Bw. Assenga amesema benki imeweza kuvijengea uwezo vikundi 336 vya wakulima wadogowadogo vyenye jumla wa wanachama 44,400 katika Mikoa ya Iringa, Morogoro na Tanga ili viweze kukopeshwa na Serikali pamoja na kutumia fedha hizo kwa ajili ya shughuli za kilimo na sio vinginevyo.
“Kupitia mafunzo hayo TADB imewezesha jumla ya vikundi 19 kutimiza masharti na maandalizi ya msingi ya kuweza kukopa; Vikundi vingine vilivyobaki vinaendelea kupatiwa mafunzo ili viweze kufikia hali ya kuweza kukopesheka hivyo kusaidia katika upatikanaji wa mali ghafi zitakazotumika katika viwanda vyetu,”alisema Bw. Assenga.
Bw. Assenga ameongeza kuwa TADB imeweza kuinua idadi ya wakulima watumiao huduma za kibenki na vyombo vya fedha wapatao 2,359 ambao kati yao wanawake ni 863 sawa na asilimia 36.6 ya wanufaika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila amesema,TADB itatekeleza kwa vitendo juhudi za Serikali za Kujenga Uchumi wa Viwanda kwa kuhuisha uwekezaji kwenye Viwanda vidogo vidogo na vya kati vya usindikaji na uchakataji wa mazao ya Kilimo, mifugo, samaki na misitu ili kuongeza tija ya kilimo hivyo kutoa mali ghafi kwa viwanda nchini.
“Benki imepitia upya mpango mkakati wake katika kutoa mikopo ili kuwezesha kufikia wakopaji wengi zaidi ili kuweza kufikia lengo la kuleta maendeleo katika sekta ya kilimo hasa katika kuongeza tija ya kilimo hivyo kutoa malighafi kwa viwanda nchini,” alisema Bibi Kurwijila.

Bibi Kurwijila ameongeza kuwa katika kuchagiza malengo hayo, TADB imejpanga Kushirikiana na wadau mbalimbali kufanya upembuzi wa miradi ya Maendeleo ya Kilimo na Umwagiliaji nchi nzima ili kubaini mahitaji halisi ya fedha na pia kusaidi kupanga maeneo ya vipaumbele ili kuanza kutoa mikopo hasa kwa utaratibu mahsusi.
Ameyataja malengo mengine ya kimkakati ya TADB yakiwemo ya kuboresha huduma kwa kuanzisha mazao maalum ya huduma za kibenki kwa wakulima wadogowadogo kulingana na mnyororo husika wa thamani na pia kuanza huduma za zaidi kupitia taasisi za fedha zilizopo (wholesale lending and Refinancing) ili kufikia wakulima wengi zaidi.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Msajili wa Hazina, Dk. Oswald Mashindano alisema taasisi za umma zina wajibu wa kusaidia utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali ili kuleta maendeleo endelevu nchini.

No comments:

Post a Comment