Tuesday, 18 October 2016

Zitto awasilisha muswada mafuta, gesi ya Zanzibar

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe 
Dar es Salaam. Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe amewasilisha rasmi muswada binafsi wa Sheria ya Mabadiliko ya 15 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu mafuta na gesi ya Zanzibar.

Zitto amesema amefanya hivyo katika kutekeleza maazimio ya Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia wa  ACT Wazalendo uliofanyika Oktoba 2016, baada ya mjadala wa mada kuhusu Zanzibar na Katiba ya Muungano.

Zitto alisema hoja hiyo inakuwa muhimu kwa sasa kwa sababu ya kunusuru uvunjwaji wa Katiba ulio wazi.

“Kusubiri Katiba Mpya hakuhalalishi iliyopo kuvunjwa. Kwa kuwa mabadiliko ya Katiba Mpya yamekwama bila ya kauli ya Serikali kujua lini mchakato utaendelea, hii hoja yetu ni ya lazima kwa sasa katika kuhalalisha hatua ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ya kutunga sheria inayohusiana na mafuta na gesi asilia,” alisema Zitto.

No comments:

Post a Comment