Serikali imesema licha ya kushuhudia takwimu za ukuaji wa uchumi wa
taifa katika muongo mmoja iliyopita, karibu theluthi moja ya wananchi wa
Tanzania bado ni masikini wanaishi katika mazingira hatarishi.
Naibu Katibu Mkuu Ikulu, Peter Ilomo amebainisha hayo kwenye uzinduzi wa
matokeo ya awali ya tathmini ya mpango wa kunusuru kaya masikini
Tanzania TASAF unaotekelezwa awamu ya tatu, ambapo amesema wakati ukuaji
wa uchumi wa taifa unakua kwa wastani wa asilimia 7 kwa mwaka, Lakini
kiwango cha umasikini kimekuwa kikipungua kwa kasi ndogo mno..
Nao wadau walioshiriki katika utafiti huo wametoa mapendekezo kadhaa
ikiwemo kuwepo haja ya kuwa na dhamira ya muda mrefu katika mpango ili
kuendeleza kizazi cha vijana chenye afya na elimu bora.
No comments:
Post a Comment