Thursday, 20 October 2016

Walima nyanya Ilula hatarini kufilisiwa

Kilolo. Kukosekana  kwa  soko la uhakika la nyanya nchini kumechangia kusuasua kwa urejeshaji wa mikopo kwa baadhi ya  wakulima katika taasisi za fedha.
Wakulima wa zao hilo katika Tarafa ya Mazombe mji mdogo wa Ilula wilayani Kilolo, Mkoa wa Iringa, .
Mkulima Rajabu Juma alisema wakazi wa Ilula wanategemea kuendesha maisha kwa kilimo cha nyanya.
Alisema wanajishughulisha na kilimo hicho kwa kutegemea mikopo kutoka taasisi za kifedha na hali ya masoko inapokuwa mbaya wanashindwa kuirejesha kwa wakati.
Mkulima wa nyanya, Upendo Sanga alisema alichukua mkopo wa zaidi ya Sh2 milioni na kuzielekeza shambani lakini  kutokana na zao hilo kukosa soko, ameamua kuziacha shambani kwa sababu hakuna wanunuzi.
Meneja Mikopo wa Mazombe Saccos,  Longino Ngwada alisema mikopo hairejeshwi kwa wakati kwa sababu   wakulima wamekosa masoko ya nyanya.

No comments:

Post a Comment