Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa
Mgwatu(kushoto) akisikiliza taarifa kuhusu kituo cha TEMESA Mkoa wa
Shinyanga kutoka kwa Meneja wa TEMESA Shinyanga Mhandisi Riziki Lukali,
alipotembelea kituoni hapo katika ziara yake katika vituo vya TEMESA
Kanda ya Ziwa.
Mtendaji Mkuu TEMESA Dkt. Mussa
Mgwatu akikagua chumba cha kuhifadhia vipuri vya matengenezo ya magari
TEMESA Mkoa wa Shinyanga, alipotembelea kituoni hapo katika ziara yake
katika vituo vya TEMESA Kanda ya Ziwa.
Mtendaji Mkuu TEMESA Dkt. Mussa
Mgwatu (wa pili kulia) akitoa maelekezo kwa watendaji wa kituo cha
Shinyanga alipotembelea kituoni hapo katika ziara yake katika vituo vya
TEMESA Kanda ya Ziwa.
Mtendaji Mkuu TEMESA Dkt. Mussa
Mgwatu (menye shati la rangi ya bluu)akiangalia gari la TANESCO
Shinyanga, linaloshikiliwa na TEMESA Shinyanga kwa sababu ya deni la Sh
Millioni 96 kushoto ni Meneja wa TEMESA Shinyanga Mhandisi Riziki
Lukali.
Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Shinyanga.
Na Theresia Mwami TEMESA Shinyanga
Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA
Mkoa wa Shinyanga inazidai Halamashauri, Mashirika na Taasisi za
Serikali mkoani humo jumla ya shillingi 163,269,269.82 kutokana na
kupata huduma ya matengenezo ya magari.
Katika taarifa yake kwa Mtendaji
Mkuu wa TEMESA, Meneja wa TEMESA Shinyanga Mhandisi Riziki Lukali
amesema madeni hayo ni ya mwaka wa fedha 2016/2017 na wamesha wasilisha
madai yao kwa wahusika na wanasubiri kulipwa.
Mhandisi Riziki Lukali aliwataja
wadaiwa hao kuwa ni TANROADS Shinyanga Sh 24,193,733.21, TANESCO
Shinyanga Sh Milioni 96,267,987.63, DED Kishapu Sh 6,753,735.03, RAS
Shinyanga Sh 2,742,097.36, KUWASA Kahama Sh 9,855,714, KASHUWASA
Shinyanga Sh 1,992,430, TBA Shinyanga Sh 5,103,062.56, Mahakama Kuu
Shinyanga Sh 5,470,628.91, Uhamiaji Shinyanga Sh 896,333.63, DAS Kishapu
Sh 1,071,573.57, NSSF Shinyanga Sh3,798,184 pamoja na RMO Shinyanga
shilingi 5,123, 789.92 milioni na jumla ya madeni hayo yote ni Sh
163,269,269.82.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amefurahishwa na
utaratibu wa TEMESA Shinyanga wa kuzuia magari ya taasisi, halmashauri
na mashirika yanayodaiwa na kituo hadi hapo yatakapolipiwa gharama za
matengenezo.
Na pia amemuagiza Meneja wa TEMESA
Shinyanga kutoa taarifa kwake kama kuna Taasisi za Serikali ambazo
hukiuka Sheria kwa kutopeleka magari yake kwenye karakana za TEMESA na
kupeleka magari hayo kwenye karakana binafsi zilizomo mkoani humo ili
hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
Dkt Mgwatu amesisitiza watumishi
kuendelea kujituma kufanya kazi kwa weledi na kwa ubora zaidi ili
karakana iweze kuvuta wateja wengi na kuongeza pato la kituo.
Aidha TEMESA Shinyanga kwa mwaka
wa fedha wa 2016/2017 kituo kimepanga kukusanya jumla ya Sh 458,160,000
kutokana na madeni na huduma zinazoendelea kutolewa kituoni hapo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yupo katika ziara ya kutembelea vituo
vya TEMESA vilivyopo Kanda ya Ziwa ili kubaini changamoto mbali mbali
zilizomo na kuzitafutia ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment