Vyoo hivyo vimezingirwa na msitu
China imezidisha matumizi yake ya vioo kuunda vivutio vya kitalii kwa
kujenga choo cha vioo ambacho mtu anaweza akaona nje na hata ndani.Vyoo hivyo, vimejengwa karibu na Ziwa Shiyan, katika mkoa wa Hunan kusini mwa nchi hiyo.
Vioo hivyo vinawezesha wanaovitumia vyoo hivyo kutazama mandhari ya kuvutia ya msitu au wengine wanaotumia vyoo jirani.
Aidha, walio nje wanaweza kuona walio ndani ya vyoo.
Kuta za vyoo hivyo, hata zile zinazotenganisha vyoo vya wanawake na wanaume, ni za vioo kabisa ingawa vioo hivyo vimetiwa ukungu kiasi.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema ni watu wachache sana waliotumia vyoo hivyo siku ya kuzinduliwa kwake.
Licha ya umaarufu wa mijengo ya kutumia vioo katika ujenzi, hasa kwenye madaraja na barabara, baadhi ya miradi imefungwa.
Mfanyakazi akifanya usafi kwenye vyoo hivyo
Vyoo hivyo vinapatikana eneo la milimani
Ejike Nnadi, akichangia ujumbe wa Facebook wa runinga ya taifa CCTV amesema: "Hapana".
Lakini kunao wengine wanaosema wanaweza kujaribu kuvitumia.
Kuna njia ya vioo iliyojengwa juu mlimani Tianmen
Tina Chen anasema mradi huo wa vyoo ni ishara kwamba kuna mtu alikuwa na pesa za "kupoteza".
No comments:
Post a Comment