Zabibu moja kiati ya mazao yayotumika kutengenezea mvinyo
Uzalishaji wa mvinyo unatarajiwa kuendelea kushuka kwa miaka
minne mwaka huu, kufuatia hali mbaya ya hewa kuathiri uzalishaji wake
katika mataifa ya Ufaransa na Amerika ya Kusini.
Shirikisho la Kimataifa la Biashara ya Mvinyo (OIV), linakadiria
uzalishaji wa mvinyo kufikia hektolita milioni 259.5 mwaka huu, ikiwa ni
kushuka kwa asilimia 5 ikilinganishwa na mwaka jana.
Shirika hilo limesema mwaka huu utakuwa wenye uzalishaji duni wa mvinyo
kuwahi kutokea tangu mwaka 2000, lakini limesema hali hiyo haitoathiri
bei ya mvinyo duniani.
No comments:
Post a Comment