Sunday, 23 October 2016

‘Upungufu wa mizigo bandarini ni tatizo’

  Wamiliki wa malori wamesema ni vigumu kuwarejesha wenye mizigo waliokuwa wakitumia Bandari ya Dar es Salam kwa kuwa wamehamia bandari za Mombasa na Beira.
Kauli ya wafanyabiashara hao inatofautia na ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage aliposema upungufu wa mizigo ni tatizo la muda duniani.
Waziri Mwijage amesema hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Malori (Tatoa), alipowaeleza hali ya kupungua mizigo inaweza kuchukua mwaka na zaidi na kuwataka wafanyabiashara hao kuwa wavumilivu katika kipindi hiki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya NMC Tracking, Natal Charles amesema itachukua muda mrefu kuwarejesha watumiaji wa Bandari ya Dar es Salaam kwa sababu waliondoka kwasababu ya ushindani wa kibiashara uliopo kwenye bandari nyingine.

No comments:

Post a Comment