wagombea Urais Marekani katika mdahalo
Wagombea Urais nchini Marekani Donald Trump na Hilary Clinton
wamechuana tena katika awamu ya tatu na ya mwisho ya mdahalo mjini Las
Vegas, ikiwa zimebaki siku chache tu, kufanyika uchaguzi nchini humo.Wamepambana vikali katika masuala mbalimbali ikiwemo umiliki wa silaha, utoaji mimba na uhamiaji haramu.
Na moja kati ya eneo waliovutana ni kuhusu uhusiano kati Marekani na Urusi na silaha za nyuklia.
Wakati Donald Trump akionyesha kuna haja ya uhusiano na Urusi na rais Vladmir Putin, Hillary Clinton anaona Urusi ni hatari kwa Marekani na hata kutupiana maneno makali.
Kuhusu umiliki wa Silaha mgombea urais wa Democratic amesisitizia msimamo wake kuhusu sheria kali katika umiliki wa silaha.
Kwa upande wake Donald Trump alimshutumu Bibi Clinton kwamba amejinufaisha kwa fedha zisizo halali.
No comments:
Post a Comment