Sunday, 2 October 2016

Sikika yataka MSD iwe taasisi huru

Image result for sikika
 
  Taasisi ya Sikika imeshauri Bohari Kuu ya Dawa  (MSD) iachwe iwe taasisi huru itakayofanya maamuzi yake yenyewe na kukusanya mtaji kushindana na wauzaji wengine binafsi wa dawa nchini.                      
Mkurugenzi wa Sikika, Irenei Kiria amesema utaratibu huo utasaida kuondoa uhaba wa dawa nchini
Ameitaka Serikali ifute ulazima wa hospitali na vituo vya afya vya umma kuagiza dawa MSD, badala yake viachwe huru kuamua kununua kutoka kwa muuzaji yeyote mwenye dawa.

Vilevile, amesema Serikali inatakiwa ihakikishe fedha zinazotengwa kwa ajili ya dawa muhimu na vifaa tiba zinapelekwa moja kwa moja kwenye akaunti za vituo au halmashauri badala ya kupelekwa kwenye akaunti za vituo zilizopo MSD.                      

Katika mkutano wake na wanahabari Jumapili leo, Kiria ameitaka Tamisemi iimarishe na kusimamia uwezo wa vituo vya kutolea huduma za afya katika halmashauri ili kujiendesha vyenyewe na wizara ya Afya ijikite katika kusimamia ubora na udhibiti wa bei za dawa.  

No comments:

Post a Comment