Serikali imewataka wanawake wachimbaji wadogo wa madini kuwa na umoja ili kuboresha kazi zao na changamoto zinazojitokeza.
Akifungua mkutano wa kazi wa wadau unojadili namna ya bora ya kuratibu na kuimarisha vyama vya wanawake wachimbaji wadogo wa madini nchini Jijini Dar es Salaam jana, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amesema kuwa serikali inatambua changamoto
zinazowakabilia wachimbaji hao na kuzitaja kuwa ni pamoja na ukosefu wa mitaji, vifaa vya kisasa, teknolojia, elimu ya masoko, uelewa mdogo na ujuzi katika sekta ya madini. Hotuba yake ilisomwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Profesa Justin Ntalikwa.
Waziri Muhongo amesema serekali inatambua mchango mkubwa wa wachimbaji hao wadogo katika sekta ya madini na kueleza dhamira ya serikali ya kuendelea kushirikiana na vikundi na vyama vya wachimba hao wanawake.
Mkutano huo unajadili matokeo ya utafiti uliofanywa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC) kwa kushirikiana na Taasisi ya Kimataifa ya UN Women Ofisi ya Tanzania.
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,Bi. Beng’i Issa, amesema utafiti umebaini kuwa ushiriki wa wananke katika sughuli au biashara za sekta ya madini ni mdogo na wachimbaji wanakabiliwa na changamoto nyingi.
Amesema utafiti umesaidia kuvitambua vyama vya wanawake wachimbaji wadogo wa madini nchini na kuainisha changamoto wanazokabiliana nazo.
Mapendekezo ya kutoka majadiliano ya mkutano huo yatachukuliwa na serikali kupitia Baraza ilitachukua matokeo ya mkutano huu wa kazi na kuyafikisha serekalini ili yatumike kwa maendeleo ya sekta madini.
Afisa Miradi Programu ya Kuwezesha Wanawake Kiuchumi wa Taasisi ya Kimataifa ya UN Women, Ofisi ya Tanzania, Bi. Tertula Swai, amesema sasa hivi kuna ushindani mkubwa wa masoko katika sekta ya madini na kuongeza kwamba utafiti huu umelenga kuwapa elimu wachimbaji ya kuweza kukabiliana na ushindani huu.
Meneja Mkuu wa Mbalawala Women Organization kutoka Mbinga Mkoani Ruvuma,Bi. Leah Kayombo,amesema shirika lao limefanikiwa kutengeneza mkaa wa kupikia kwa kutumia makaa ya mawe ya Ngaka Mbinga ili ku kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya mkaa.
No comments:
Post a Comment