Na Mwandishi Wetu Dodoma.
Mapema Septemba 2016 kwa mara ya
kwanza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses
Nnauye aliwasilisha kwa mara ya kwanza Bungeni Muswada wa Sheria ya
Huduma za Habari na kuanza kujadiliwa na kutolewa maoni kutoka kwa wadau
mbalimbali wa Habari nchini.
Kwa sasa Muswada huu unaendelea
kujadiliwa na kuchambuliwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na
Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Peter Serukamba na
baada ya mchakato huo kukamilka utapelekwa kwa ajili kuanza kujadiliwa
na wabinge.
Sasa hoja yangu naielekeza katika
kuangalia Muswada huu hasa katika sehemu ya Tatu (c) Uthibitishwaji wa
wanahabari kifungu cha 18 (1) na (2) vinaelezea kuwa Mtu hataruhusiwa
kufanya kazi za uandishi wa habari isipokuwa kama mtu amethibitishwa na
Sheria hii na (2) inasema mtu ambaye anakusudia kufanya kazi ya uandishi
wa habari ataomba kuthibitishwa na Bodi kwa utaratibu wa maombi
utakaoainishwa katika kanuni.
Ukisoma kifungu hiki na sehemu
zake zote utaona kuwa lazima kutakuwa na vigezo ambavyo mwandishi wa
habari atapaswa kuwa navyo ili Bodi iweze kumthibitisha kuwa mwandishi
wa habari kamili na baadae kumpatia Press Card.
Tukiangali kwa mifano tu ya
taaluma ambazo watu wake wanapata udhititisho kutoka kwa Bodi zao utaona
kuwa hata vigezo vyenye ngazi fulani ya kitaaluma na kwa mfano
wanasheria ili kudhititishwa kuwa mwanasheria na kupata mhuri wa kuwa
Wakili unabidi uwe na Shahada ya Kwanza ya Sheria na kufanya baadhi ya
mitihani ya kufuzu ili kudhitishwa.
Kwa waandishi wa Habari pia
tutegemee kuwepo kwa vigezo na masharti ambayo kwa vitahitaji kuongeza
elimu tulizonazo katia fani yetu na pia hili litasababisha sasa vyuo vya
uandishi wa habari na mawasiliano kutoa elimu iliyo bora zaidi ili
kuendana na mabadiliko haya.
Tumeshudia uwepo wa vyuo vya
uandishi wa habari kila sehemu hata vingine ukiangalia mazingira yake
lazima utilie shaka kama vinatoa ile elimu inayostahili na
iliyodhibitishwa na mamlaka zilizopo za TCU na NACTE.
Niwaombe tu wahusika katika vyuo
vya uandishi wa habari kuzingatia vigezo na masharti ya utoaji wa elimu
ya Habari na Mawasiliano katika vyuo vyao kwani kuja kwa Sheria ya
Huduma za Habari ni mwanzo wa kuifanya taaluma ya habari kuwa taalum
inayoheshima na kuwa taaluma inayoheshimika sana na sio rahisi kuipata
kama sasa watu wanavofikiria tu ukitaka kuwa mwandishi wa habari unaweza
kusoma miezi mitatu hivi basi umekuwa mwandishi wa habari.
Ingawa kuna baadhi watu wanasema
wanatumia vipaji vyao vya uandishi wa habari na utangazaji lakini tujue
kuwa kipaji bila ya kuendelezwa ni kazi bure tunahitaji kuviendeleza
vipaji hivyo kwa kupata elimu na ujuzi zaidi wa fani ya habari ili
kuendana na mabadiliko ya teknlolojia na Sheria za nchini.
No comments:
Post a Comment