Wednesday, 19 October 2016

Mmarekani aliyemponda glasi ya bia Msomali aliyezungumza Kiswahili ahukumiwa kifungo cha miezi 6 jela

Jama akiongea na waandishi wa habari baada ya hukumu kutolewa
  Mmarekani aliyemponda na glasi ya bia mwanamke wa Kisomali kwakuwa alimsikia akizungumza Kiswahili, amepatikana na hatia.
Tukio hilo lilitokea mwaka jana huko, Minnesota.
Jodie Marie Burchard-Risch alishtakiwa kwa kumshambulia Asma Jama, mhamiaji wa Kisomali kwenye mgahawa mmoja October 2015. Jama na familia yake walikuwa wamekaa kwenye mgahawa na walikuwa wakizungumza Kiswahili, lugha ambayo huizungumza wanapokuwa na watoto ili wasielewe baadhi ya vitu.


 Wakati kundi hilo likipita karibu na Burchard-Risch, aliwaambia “In America, we speak English.”
Jama alisema alipuuzia maneno hayo kabla ya mambo kuchemka zaidi pale Burchard-Risch alipomwambia kwa sauti kubwa arudi nchini mwake.
Baadaye Burchard-Risch alichukua glasi kubwa na kumpiga nayo usoni na kukimbia. Jama alijeruhiwa mdomo na alishonwa kwa nyuzi nyingi.

 Jama alishonwa nyuzi nyingi baada ya kujeruhiwa
Burchard-Risch amehukumiwa kifungo cha siku 180 jela na miaka mitano ya uangalizi. Pia atatakiwa kulipa fidia.
Jodie Marie Burchard-Risch

No comments:

Post a Comment