Sunday 16 October 2016

Mbunge wa jimbo la chalinze ridhiwani kikwete achangia damu,atembelea wananchi wake na kusikiliza kero zao.

 Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa katika zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya Mama na mtoto,jimboni humo.

 Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akisikiliza mmoja wa kina mama aliyesimama kuzungumza kuhusu kero wanazopata katika shughuli zao za kifugaji .

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji aliyesimama akizungumzia athari zizokanazo na sheria namba 10 ya mwaka 2010 katika kikao na Mbunge wa jimbo la Chalize Ridhiwani Kikwete.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,ameshiriki katika zoezi la kuchangia damu linalotambulika ‘’Changia Damu Salama kwa Mama na Mtoto’’lilifanyika jimboni humo ili kusaidia upatikanaji wa damu salama.

Akizungumza katika zoezi hilo Ridhiwani amesema kuwa amevutiwa na zoezi hilo na kuamua kujitolea kuchangia damu ili kumkomboa mama na mtoto.Katika tukio lingine Ridhiwani amekutana na kufanya mazungumzo na wakinamama wa jamii ya wafugaji wa kabila la wa Maasai ili kuangalia ni namna gani atasaidia kutatua changamoto zinazowakabili wafugaji katika jimbo hilo.

Aidha amepata nafasi ya kutembelea Lambo la maji lililojaa matope katika eneo la Pera ili kujionea hali halisi ya eneo hilo ili kusaidia kurudisha lambo hilo katika hali yake ya kawaida.

No comments:

Post a Comment