Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi wa awali ya Umoja wa Mastaifa.
Uchunguzi huo uliofanywa kwa pamoja na ofisi ya haki za binadamu ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini DRC MONUSCO, imeorodhesha wahanga 422 wa ukiukwaji wa haki za binadamu ukijumuisha haki ya kuishi, uhuru na usalama wa watu, uhuru wa kukusanyika kwa amani na kujieleza.
Watu 48 kati ya 53 waliopoteza maisha waliuawa na vyomvo vya serikali ikiwemo polisi na 38 ambao miongoni mwao walipigwa risasi kichwani, kifuani na mgongoni.
Ravina Shamdasani ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu Geneva amesema ukwepaji wa sheria kufuatia ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo, kupiga risasi, kukatakata na ukamataji wa kiholela imekuwa ni janga kubwa nchini DRC kwa miongo mingi.
No comments:
Post a Comment