Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Mashindano ya mchezo wa Golf ya PWC
Trophy yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumamopsi Oktoba 22 katika uwanja
wa Golf wa Lugalo yanatarajiwa kutumika kuchuja Wachezaji wa Timu ya
Taifa ya golf wanaotarajia kushiriki mashindano ya East Afrika Challenge nchini Ethiopia.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Jeshi la Wananchi wa
Tanzania ya Lugalo Jijini Dar es Salaam yatakapofanyika mashindano hayo
Brigedia jenerali Michael Luwongo na kuongeza kuwa ni heshima kubwa kwa
klabu.
“ Ni
Heshima Kubwa kwa Klabu yetu kupokea mashindano ya PWC lakini ni
heshima kutumia mashindano hayo kupima uwezo wa wachezaji waliochaguliwa
timu ya taifa na mchujo wa wachezaji ili kupata idadi kamili ya wachezaji wanaotarajiwa kuwakilisha nchi.” Alisema Brigedia Jenerali Luwongo.
Alisema
maandalizi yote yamekamilika ikiwa ni pamoja na wachezaji kutoka Klabu
zote za golf nchini ambao mpaka sasa wamefikia zaidi ya 100 ambao
wamethibitisha kushiriki na kuomba wadhamini zaidi kuendelea kujitokeza
kusaidia mchezo wa golf kupitia Lugalo kwani Milango iko wazi.
Kwa Upande wake Nahodha wa Klabu ya Lugalo Japteni Masai alisema mashindano yanatarajiwa kuanza saa moja na nusu ambapo wachezaji wa Kulipwa,Wachezaji wa Timu ya Teule ya Taifa,Junior na wanawake wataanza.
Kapteni Masai aliongeza kuwa kundi la Pili la mashindano hayo yatakayoendeshwa kwa mtindo wa Mikwaju ya Jumla Stroke Play Net litaanza saa tatu asubuhi ambapo Wachezaji wa Ridhaa wote kwa makundi yote watacheza.
Kwa Upande wake Afisa Masoko wa PWC ambao
ndio wadhamini wa mashindano hayo Wilfred Nyaki alisema wanashukuru
kupata fursa katika mashindano haya na wamechagua klabu ya lugalo kwa
kuwa ni klabu bora nchini na wataendelea kufanya hivyo ikiwa sasa ni
miaka mitatu nawanadhamini ili kutoa nafasi kukuza mchezo huo miongozi
mwa jamii.
Nyaki
aliongeza kuwa Maandalizi yote kwa Upande wa zawadi yamekamilika na
kinachosubiriwa ni washindi kukabidhiwa na wanamatumaini makubwa na
mafanikio ya siku hiyo ikiwemo Timu ya Taifa kupata wachezaji
waliowakusudia.
Wachezaji wa Timu ya Taifa watakaothibitishwa baada ya mashindano ya PWC wanatarajiwa kuondoka nchini Jumanne Oktoba 25.
No comments:
Post a Comment