Saturday, 1 October 2016
Mageti ya uwanja wa Taifa yamevunjwa na mashabiki
Mashabiki waliofurika katika mageti walishindwa kuingia uwanjani kutokana na mashine kushindwa kufanya kazi vizuri na kusababisha wavunje mageti mawili.
Mashabiki wamevunja mageti la upande kushoto kutokea chuo cha Duce na kuingia ndani jambo linalowalazimisha polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.
Mashabiki hawaelewi wanadai wamepanga foleni kwa muda mrefu, lakini hakuna kinachoendelea. Wengine wanataka kuingia uwanjani kwa kuonyesha kadi tu za selcom, lakini wanakataliwa.
Labels:
MICHEZO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment