Miongoni mwa Wakurugenzi aliodai Lipumba kuwateua ni pamoja na;
Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha -Thomas Malima
Maftaha Nachuma - Mkurugenzi wa Mambo wa Nje CUF
Zaynab Mndolwa -Mkurugenzi wa Haki za Binadamu
Jaffari Mneke -Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi.
Hata hivyo, Lipumba amedai kuwa, aliowateua watakaimu nyadhifa hizo hadi watakapothibitishwa na Baraza Kuu la Uongozi Taifa la CUF.
Aidha, amedai kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje atamteua kutoka Zanzibar hapo baadae.
Sambamba na hilo, alisema wakurugenzi na manaibu wakurugenzi aliowateua baada ya mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika Juni, 21, 2014 wataendelea na nyadhifa zao huku akitishia kuwa, ikimbidi kufanya mabadiliko ya wakurugenzi hao hatosita kufanya hivyo.
Katika hatua nyingine, Lipumba alitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha CUF ambaye ndiye Katibu wa Bodi ya Wadhamini kuitisha kikao cha bodi hiyo Oktoba 4,2016 ili ipewe taarifa ya msimamo na ushauri wa Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi kuhusu mgogoro wa uongozi kitaifa wa CUF.
Lipumba alisema kuwa, amefanya teuzi za wakurugenzi hao kwa mujibu wa katiba ya CUF ya mwaka 1992 toleo la 2014 ibara ya 90 (1) (f) ambayo inasema kuwa Mwwenyekiti Taifa atateua Wakurugenzi na Manaibu Wakurugenzi kutoka miongoni mwa wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa au wanachama jasiri wa chama.
No comments:
Post a Comment