“CONGO TUTAWAZIKA HAPA”Ndivyo
anavyoonekana kusema Mshauri wa Maendeleo ya soka la Vijana, Kim Poulsen
(kushoto) akimwelezea Mkuu wa Msafara wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye
umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, Ayoub Nyenzi kwenye Uwanja
wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo.
Uwanja huo ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa
jijini Brazzaville ndio utakaotumika kwa ajili ya mchezo wa kuwania
kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kati ya Tanzania na Congo,
Jumapili Oktoba 2, 2016.
Huyo ndiye Muhsin Malima Makame
au unaweza ukamwita ‘Super Sub’ wa Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa
chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, akikokota mpira kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo
kuonyesha uwezo wake uwanjani pindi anapoingia kipindi cha pili kuokoa
jahazi. Akikosa kufunga huwa ni kama bahati mbaya.
Beki wa kushoto wa Timu ya Taifa
ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, Nickson
Kibabage akimdhibiti Kelvin Nashon wakati wa mazoezi ya timu hiyo
yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat
– Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
Kiungo wa Timu ya Taifa ya Vijana
wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, Kelvin Nashon
‘akisepa na kijiji cha mabeki’ wakati wa mazoezi ya timu hiyo
yaliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat
– Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
Libero wa Timu ya Taifa ya Vijana
wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, Ally Msengi (Kulia)
akimiliki mpira huku Mshambuliaji wa timu hiyo, Ibrahim Abdallah
akipigia hesabu mpira huo wakati wa mazoezi yaliyofanyika leo kwenye
Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa
Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
Baadhi ya vigogo wa Timu ya Taifa
ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, kutoka
kushoto ni Dk. Gilbert Gilbert Kigadye, Mratibu wa timu, Pelegrinus
Rutayuga na Dk. Sheicky Mngazija wakifuatilia mazoezi hayo kwenye Uwanja
wa Kumbukumbu ya Alphonse Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo
kabla ya mchezo wa Jumapili.
Kipa Na. 1 wa Timu ya Taifa ya
Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 – Serengeti Boys, Ramadhani
Kabwili akifanya vitu vyake kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Alphonse
Massamba-Débat – Rais wa zamani wa Congo kabla ya mchezo wa Jumapili.
No comments:
Post a Comment