Saturday, 1 October 2016

Jaji mkuu atimuliwa kwa kutotoa vyeti vya ndoa za jinsia moja

 Ray Moore aliagiza kwamba wapenzi wa jinsia moja wanyimwe vyeti vya ndoa, hata baada ya uamuzi wa kihistoria mwaka jana, uliohalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Jimbo la Alabama, nchini Marekani, limemwondoa kazini jaji mkuu aliyekaidi uamuzi wa mahakama ya juu kuhusu ndoa za jinsia moja.

Ray Moore aliagiza kwamba wapenzi wa jinsia moja wanyimwe vyeti vya ndoa, hata baada ya uamuzi wa kihistoria mwaka jana, uliohalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja.


Ametaja uamuzi wa kuondolewa kwake kama kampeni ya makundi ya wapenzi wa jinsia moja, ya kuendeleza ajenda iliyo kinyume na maadili.

Kundi la wanaharakati lililompeleka mahakamani linasema kwamba alikabidhiwa wadhfa wake kama jaji mkuu wala sio mchungaji.

Bwana Moore, anafahamika na wengi kwa hatua yake ya kujenga mnara wa amri kumi za Bibilia kwenye majengo ya mahakama ya jimbo hilo, amekuwa akizungumza kwa uwazi dhidi ya ndoa za jinsia moja.

Jaji huyo pia kwa wakati mmoja aliwataka majaji wa jimbo la Alabama kutotoa vyeti vya ndoa kwa wapenzi wa jinsia moja, kinyume na uamuzi wa mahakama ya juu nchini Marekani.

Ndoa za wapenzi wa jinsia moja ni halali nchini Marekani

No comments:

Post a Comment