Akizungumzia kampeni hiyo, Meneja Msaidizi wa Hospitali ya Sanitas, Dk. Sajjad Fazel alisema hospitali yao imeanzisha kampeni ya Pink Oktoba ili kuwasaidia wananchi kupata huduma ya kupima saratani ya matiti kwa urahisi bila kuwa na gharama zozote.
“Huu mwezi wa Oktoba sababu ni mwezi maamulu wa saratani duniani, tutakuwa tunafanya vipimo kwa mtu kuja kumuona daktari kwa ajili ya kujua kama ana saratani ya matiti bure kabisa bila kutoa pesa yoyote,” alisema Dk. Fazel.
Kwa upande wa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Afya ya Mama na Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Dk. Felix Bundala alisema licha ya serikali kufanya jitihada mbalimbali za kukabiliana na ugonjwa wa saratani ya matiti lakini bado kuna changamoto ya wananchi kutokujitokeza kupima ugonjwa huo.
Dk. Bundala alisema ni vyema wananchi wakajitokeza kwa wingi kupima saratani ya matiti kutoka hospitali ya Sanitas kwa siku ambazo watakuwa wanatoa huduma ya kupima bure ili waweze kujua hali zao za kiafya na hatua ambazo wanapaswa kuzichukua.
“Ingawa inaonekana jamii yetu ina ufahamu kuhusu saratani ya matiti, lakini sio wengi waokwenda kufanyiwa vipimo, serikali imekuwa ikitumia vyanzo vyake vya ndani kuwashauri wananchi wapime huu ugonjwa maana hata takwimu zinaonyesha hadi mwaka 2020 ongezeko la wagonjwa wa saratani ya matiti itazidi kuongezeka,
“Ni vyema kufanyiwa uchunguzi mapema sababu wakija tayari wapo kwenye hatua kubwa inakuwa ngumu kuwatibu, tuwashauri wananchi wawe na tabia ya kufanya uchunguzi mara kwa mara,” alisema Dk. Bundala.
No comments:
Post a Comment