Mwakilishi
Mkazi wa shirika la linaloshughulika na masuala ya Afya ya Uzazi na
Uzazi wa mpango kwa Wanawake na Wasichana la EngenderHealth Richard
Killian( katikati) akizungumza na Waziri wa Afya ,Maendeleo ya
Jamii,jinsia,Wazee na Watoto mapema leo kwenye ofisi ya waziri
huyo,Kushoto ni Rais na Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo bi. Ulla
Muller na kulia ni Waziri Ummy Mwalimu.
Rais na Mkurugenzi wa
EngenderHealth Bi. Ulla Muller (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo
wakati alipomtembelea waziri wa afya na kuzungumza mikakati yao katika
upande wa afya,rais huyo atatembelea Mkoa wa Manyara
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya
jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy mwalimu akiongea na Rais pamoja na
Mwakilishi mkazi wa Shirika la EngenderHealth walipomtembelea ofisini
kwakwe. Waziri Ummy amesema hivi sasa asilimia 27 ya wanawake wa
Kitanzania ndio wanaotumia njia za uzazi wa mpango ambapo serikali
ilijiwekea malengo mwaka 2012 kwamba ifikapo mwaka 2020 ifikie asilimia
50 ya matumizi ya njia ya uzazi wa mpango( Picha na Wizara ya Afya)
No comments:
Post a Comment