Saturday 15 October 2016

Benki imetetea matumizi ya Dola

Image result for benki kuu ya tanzania
Benki kuu Tanzania (BoT), imesema matumizi ya fedha za kigeni kama vile dola, pauni na Euro, hayasababishi kushuka au kuifanya shilingi ya Kitanzania kutetereka.
Badala yake BoT imesema sababu za kushuka au kuyumba kwa sarafu ya nchi, mbali na mfumuko wa bei ni nakisi ya mapato na matumizi ya nje ya nchi.

Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi, Johnson Nyella, alisema hayo baada ya Nipashe kutaka kujua benki hiyo imetekelezaje agizo la aliyekuwa Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, alilolitoa bungeni mwaka 2007 kutaka miamala yote ya kibiashara isifanyike kwa fedha za kigeni, ikiwamo dola.

Nyella alisema kushuka kwa shilingi hakusababishwi na matumizi ya dola kama imani iliyojengeka miongoni mwa Watanzania.

No comments:

Post a Comment