Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus Likwelile akitiliana
saini na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya Exim ya China Bw. Zhu
Ying kuhusu makubaliano ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango
cha kisasa (Standard Gauge), jijini Dar es Salaam,
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus Likwelile
akibadilishana hati ya makubaliano na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki
ya Exim ya China Bw. Zhu Ying mara baada ya kusaini makubaliano ya
awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge),
jijini Dar es Salaam,
Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania leo imetiliana saini na Benki ya Exim ya China makubaliano
ya awali ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard
Gauge).
Makubaliano hayo ya awali
yamefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servaciaus
Likwelile kwa niaba ya Tanzania na Naibu Meneja Mikopo Nafuu wa Benki ya
Exim ya China Bw. Zhu Ying.
Akizungumza katika hafla hiyo ya
utiliaji saini Dkt. Likwelile amesema hatua hiyo inawezesha hatua za
upembuzi yakinifu, usanifu na uundwaji wa timu za pamoja kuanza kuanisha
mahitaji halisi ya ujenzi wa mradi huo.
Zaidi ya Shilingi Trilioni 16 za
Tanzania zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa mradi wa reli ya kati
yenye urefu wa Kilometa 2,190 ambapo Benki hiyo itashirikiana na
Serikali ya Tanzania katika ujenzi wake.
Mradi wa ujenzi wa reli ya kati
utahusisha ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa kutoka Dar es
Salaam-Tabora-Isaka-Mwanza na
Tabora-Mpanda-Kalemela-Uvinza-Kigoma-Isaka-Keza hadi Msongati
No comments:
Post a Comment