Monday, 18 July 2016

Namna ya Kuhifadhi Akiba Ya Fedha.

 
  Na Kalonga Kasati

Wengine huita pesa sabuni ya roho, wengine huita pesa shetani  pia pesa hiyohiyo huitwa majina mbalimbali kutokana na matumizi ya sehemu mbalimbali, mfano pesa huitwa zaka, sadaka, ada, kodi, mchango, nauli, , bili na mengineyo mengi ila majina  yote hayo humanisha pesa. Pesa ambayo kila mtu anautafuta kwa udi na uvumba, usiku na mchana.
Tuanze moja kwa moja kuangalia maada yetu, kabla kalamu yangu haijaisha wino. Somo la kuweka akiba kwa tulio wengi ni changamoto kubwa sana. Hata hivyo kutokana na ugumu huo wa kuweka akiba ndio ambao unatafanya tuzidi kuwa na maisha yaleyale kila siku.


Pia kuna usemi unasema ukifanya jambo lile lile kwa njia ile hata matokeo yake huwa ni yale yale. Hata Ukifuatilia kwa umakini watu ambao tuna maisha yale yale kila siku moja ya changamoto kubwa ambayo inatuathiri ni kwamba hatuna nidhamu ya fedha na nidhamu ya muda hii ni kwasababu fedha tumeishaiona ni kitu cha kawaida sana.

Naomba tujikite zaidi kwani nataka Tuzungumze kuhusina na nidhamu ya fedha zaidi, kwa kuwa nidhamu hiyo ndio ambayo watu wengi hatunayo hata chembe.

Nidhamu hiyo hiyo ndiyo ambayo inanifanya nimkumbuke sana Mfanyakazi mwenzangu Looqman Maloto kwani aliwahi niambie ya kwamba pesa ina makelele sana, baada ya kusikia hayo nikamuuliza unamanisha nini?

Ndipo akanieleza ukichunguza mtu akipata pesa utashangaa, kwani mara nyingi hujikuta kila kilichopo mbele ya macho yake anakitaka, na kwa kuwa mtu huyo huyo hana bajeti ambayo inamuhusu utashangaa pesa hiyo ikiisha atakwambia pesa shetani kwa kuwa pesa hiyo imeisha bila kufanya chochote.

Ili kuepukana na adha ya makelele hayo hatuna budi kujua. Namna ya kuweka akiba ya fedha.

1.Tengeneza bajeti yako.
Ili uweze kuwa na nidhamu ya pesa ni lazima uwe na bajeti ambayo inaeleza kwa kina kuhusina na   pesa zako. Hata hivyo unaweza nikukumbushe ya kwamba bajeti inahusiana na mapato na matumizi ya pesa. Kwahiyo ni vyema ukawa unakuwa na utaratibu wa kuandika katika sehemu yako ya kumbukumbu kile ambacho unakipata na kile ambacho unakitoa.
Ni Lazima kila siku uwe na bajeti yako ambayo itakufanya uweze kujua yapi ni matumizi ya lazima, na yapi sio matumizi ya lazima. Pia ukumbuke ya kwamba bajeti hupangwa kabla ya kuwa na pesa mkononi.

Hifadhi chenji.
2. Hifadhi chenji.
Uhifadhi wa chenji kwa watu wengi ni suala gumu sana, hata hivyo endapo utaamua kujifanyia uchunguzi ni kiasi gani? che fedha ambacho umekihifadhi baada ya kupata huduma au bidhaa fulani utajua ukweli juu ya jambo hilo.
Mimi naamini katika kufanya uchunguzi, siku moja nilikuwa najihoji mwenyewe ni kwanini wafanyabiashara wadogo wadogo wapo sana maeneo ya vituo vya madaladala hususani maeneo mengi ya mjini?


Nikaja kugundua ya kwamba nauli nyingi za mjini huwa hazipo kamili kwa maana kwamba kwa namna kivyovyote vile mara nyingi watu hurudishiwa chenji kwenye usafiri huo.
Hivyo kwa kuwa wengi wetu somo  la chenji limepita kushoto hivyo wafanyabiashara hao huamua kukaa maeneo hayo huku wakiwa na uhakika chenji hiyo itakuwa yao maana ni lazima utatanunua vitu hivyo.

Tuachane na mfano huo tuje tuongalie maisha yetu kwa ujumla wake kwani ni asilimia chache kati nyingi ya watu ambao hutunza chenji baada ya kununua huduma/bidhaa.
Nafikiria kila mmoja wetu ambaye anasoma makala haya aweze kutafakari na kuona ni jinsi gani tabia ya uhifadhi wa chenji ambavyo unaweza kubadili maisha yake. Uhifadhi wa chenii hupelekea mtu huyo na  pia kumfanya mtu huyo kuwa na nidhamu ya fedha.

Nidhamu ya fedha ndiyo ambayo itakufanya ujenge hofu na upendo wa pesa. Hofu ya mapesa itakusaidia kwa kiwango kikubwa kujua yapi ni matumizi ya lazima na ni yapi si matumizi ya lazima. Jamii ya leo ni kizazi cha hapa kazi tu.
Niungane na kauli hiyo na kusema ya kwamba kazi tu bila matumizi sahihi ya kifedha kwa kila mtu ni sawa na bure. Hivyo nakusihi uweze kuhifadhi kila chenji kuanzia sasa.

3. Jilipe mshahara kwa kazi unayoifanya.
Hajalishi umeajiliwa au umejiajili, hili ni jambo la msingi sana kujilipa mshahara. Huenda ukawa hajanielewa ni vipi unatakiwa kujilipa mshahara, kaa vizuri kisha twende sawa, ni hivi kumbuka fedha yeyote ile inakupa hamasa za kusonga mbele kwa kufanya baadhi ya mambo yafuatayo. Mosi ni kwamba ni lazima uweze kujua ni kiasi gani unatakiwa kukitenga kwa ajili ya akiba.

Kama utakuwa si mgeni katika makala zangu nilishawahi kuandika hapo awali makala isemayo Jinsi ya kupangalia matumizi ya fedha, moja ya maelezo ambayo niliyaandika ni kwamba katika pesa ambayo unayoipata kila baada ya muda fulani ambao umejipangia ni kwamba asilimia 15 ni lazima uitenge kwa ajili ya akiba. Halafu nikukumbushe ya kwamba katika pesa ambayo inahitaji nidhamu ya hali ya juu ni pesa ya akiba.

Mwisho ni malize kwa kusema, wapo wanasema pesa mwenzake ni matumizi, hiyo ni kweli lakini pesa hiyo hiyo isifanye ipotee bure bali ifanye ukuzalishie pesa nyingi zaidi. Pia wanasema pesa ina makelele hasa pale unapoipata hivyo cha msingi pesa yoyote ambayo unaitumia hakikisha kwamba ilikuwepo katika matumizi yako
.

No comments:

Post a Comment