Hii ndiyo hoteli mpya aliyofungua Chistiano Ronaldo
FUNCHAL, Ureno
MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo hatimaye
ameifungua hoteli yake ya nyota tano ambayo inaonekana kuwa na ubora wa
kiwango cha juu hasa katika suala la ubunifu wa majengo.
Ronaldo ambaye kwa sasa yupo katika mapumziko kwenye Fukwe za Ibiza,
Hispania amekamilisha mradi huo wa hoteli ambayo ipo katika Mji wa
Madeira ambako ndipo nyumbani kwao.
Hoteli hiyo iliyopewa jina la The Pestana CR7 Hotel, ina vyumba 48 vya
kulala, gym na bwawa la kuogelea ni moja ya hoteli nne ambazo mchezaji
huyo amepanga kujenga.
Kwenye korido za hoteli hiyo kuna nyasi za bandia pamoja na jezi ya
Ronaldo ya timu ya taifa yenye namba saba ambayo ndiyo amekuwa
akiitumia.
Ndani ya vyumba kuna urembo tofauti kwa kila chumba ambapo pia kuna
michezo ya kwenye runinga ‘Play Station’ huku baadhi ya vyumba vikiwa na
bei tofauti.
Gharama ya kulala katika hoteli hiyo kwa usiku mmoja ni pauni 180 (Sh
laki 5), kuna huduma ya bure ya internet, pia kuna baadhi ya vyumba
ambavyo kutokana na ubora wake kulala kwa usiku mmoja ni pauni 575 (Sh
milioni 1.6).
Hoteli nyingine ya Ronaldo ambayo inatarajiwa kufunguliwa baadaye mwaka
huu itapatikana Lisbon, Ureno nyingine zitafunguliwa Madrid, Hispania
na New York, Marekani.
No comments:
Post a Comment