Managementi inayowasimamia wasanii hao ya Rockstar 4000 imesema wasanii hao walivamiwa wakiwa kwenye kikao cha mikakati ya kuzungumzia safari yao nchini humo watakakokaa kwa muda wa siku saba.
Chanzo hicho kimesema majambazi hao walikuwa na silaha za moto (bunduki).
Miongoni mwa vitu walivyoibiwa ni pamoja na simu zao za mkononi ambapo
majambazi hao wakati wote wa tukio waliwanyooshea bunduki kina Ali Kiba
kuwatisha zaidi na bila kutaka kupoteza muda.
Baraka Da Prince na Ali Kiba wote ni wazima wa afya na hawakudhurika kwenye hilo tukio.
Pamoja na tukio hili kutokea, wasanii hao hawatorudi nchini bali wataendelea na mipango yao iliyowapeleka nchini humo.
No comments:
Post a Comment