Wednesday, 4 May 2016

Wimbo wa Chura wa Snura Umefungiwa Rasmi Kuchezwa Katika Vyombo Vya Habari


 

 Na Mwamvita Mtanda

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Vyombo Vingine Vinavyoshughulika na Sanaa ikiwemo BASATA Wamekubaliana kuufungia Wimbo na Video Ya Chura kupigwa kwenye Vyombo vya Habari, Maeneo ya Hadhara na Mahala popote kwenye Mkusanyiko wa watu.
 
Serikali kupitia Muwakilishi wake imedai kuwa, Wimbo huo Unadhalilisha na kukiuka Haki za Binadamu.

Wizara pia imebaini kuwa Msanii Snura, hana nyaraka Maalum za kujihusisha kwenye Masuala ya Muziki, hivyo imemfungia kujihusisha na Matamasha ya aina yoyote mpaka pale Atakapotimiza Taratibu.

Msanii huyo ameamriwa kutoa Haraka Video hiyo kwenye Mitandao ya Kijamii ikiwemo Youtube, na kwa Mtu yoyote atakayeisambaza kwenye Mitandao ya kijamii atachukuliwa Hatua kali za kisheria

No comments:

Post a Comment