Monday, 16 May 2016

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon na Donald Trump waingia vitani

Donald Trump

Mgombea anaewania urais nchini Marekani Donald Trump ameonya kuwa huenda asiwe na Uhusiano mzuri sana na waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron -- Ikiwa atakuwa rais wa Marekani.

Mwezi Disemmba, Bwana Cameron alimtaja Trump kama mtu mwenye "ubaguzi, mjinga, na Mwenye makosa" kufuatia kauli yake kwamba ataweka marufuku ya muda ya kuingia Marekani dhidi ya waislam.

Bwana Cameron amekataa kufuta kauli zake dhidi ya Bilionea Trump , ambae anatarajiwa kuwa mgombea wa urais wa Marekani kupitia chama cha Republican katika uchaguzi wa 
 Mwezi Novemba.

 David Cameron

 Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron
Akizungumza katika kituo cha televisheni cha Uingereza ITV kwa mara ya kwanza mbele ya Umma tangu akosolewe Bwana Trump, alisema yeye si mjinga ama mbaguzi stupid bali ni''mugombanishi".

Kuhusu kauli za Bwana Cameron, Bwana Trump alisema : "yaelekea hatutakuwa na uhusiano Mzuri sana, nani anajua.
"Natumai kuwa na uhusiano mwema na yeye, lakini inaonekana ni kama hataki kutatua 
Tatizo."Donald Trump na meya wa London Sadiq Khan

Donald Trump ( kushoto) alimkemea pia Meya wa London Sadiq Khan (kulia)
Donald Trump pia alimkemea Meya wa London , Sadiq Khan, kwa kumuita "mjinga".
Alielezea kauli yake kama kosa na isiyokua na ya heshma, huku akimtaka Bwana Khan afanyiwe vipimo vya uwezo wa akili yake (IQ).

No comments:

Post a Comment