Na Mwamvita Mtanda
Wizara ya Ardhi ,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi imesema jumla ya Watumishi wa Serikali 210
wameidhinishiwa mikopo nyumba yenye thamani shilingi bilioni 2.3 baada
ya kukidhi vigezo vya Bodi ya Mfuko wa Mikopo ya Nyumba za Watumishi wa
Serikali.
Kauli hiyo imetolewa
leo mjini Dodoma na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Lukuwi wakati akiwasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya mapato
na matumizi kwa mwaka ujao wa fedha.
Alisema kuwa Serikli
imekamilisha uhakiki wa maombi mapya 191 ya watumishi wa umma waliomba
mkopo wa nyumba katika maeneo mbali.
Mhe. Lukuwi aliongeza
kuwa kati ya maombi hayo watumishi 181 yamekidhi vigezo vya mfuko huo
na yanatarajiwa kuidhimishwa mwishoni mwa mwezi huu.
Aidha , alisema kuwa
Serikali kupitia Watumishi Housing Company (WHC) imeanza kujenga nyumba
za kuuza kwa watumishi wa umma katika mikoa ya Morogoro, Dar es salaam,
Pwani, Tanga na Mwanza
Mhe. Lukuwi alisema
kuwa watumishi wa umma wanaotaka kununua nyumba hizo wanawaweza kupata
mikopo yenye mashrti nafuu kupitia Benki za Azania , CRDB, NMB, BoA na
Exim zilizoingia makubaliano na Watumishi Housing Company wanaojenga
nyumba kwa ajili ya kuwauzia watumishi wa umma katika maeneo mbalimbali
nchini.
No comments:
Post a Comment