Na Chrispino Mpinge
Mei
6 2016 bunge linaendelea tena Dodoma, katika kipindi cha maswali na
majibu Mbunge wa Bukombe Doto Biteko ameuliza Serikali kuwa ‘Je, kwanini
Serikali inachukua muda mrefu Sana kurekebisha mishahara ya Walimu
baada ya kupandishwa vyeo?‘
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejiment ya utumishi
wa Umma na Utawala bora ’Ni kweli kwamba miaka ya nyuma
kulikuwepo ucheleweshwaji wa kurekebisha mishahara kwa Mfumo wa taarifa
za kiutumishi na mishahara wakati huo kila mwajiri kuwasilisha Marekebisho ya watumishi wake Ofisi ya Rais‘
‘Kuanzia mwaka 2012 mfumo huu wa taarifa za kiutumishi na
mishahara uliimarishwa kutoka Toleo la 7 kwenda la 9 la Lawson ambapo
mwajiri alisogezewa huduma ya kufanya Marekebisho mbalimbali ya
kiutumishi yanayotokea katika ofisi yake bila ya kulazimika kusafiri
kwenda Dar es salaam‘
No comments:
Post a Comment