Na Mwamvita Mtanda
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Snura Mushi amesema kuwa
atajitahidi kuwaelimisha Wasanii wenzake kuandaa nyimbo zinazokwenda na
maadili ya Kitanzania Snura alisema kuwa lengo la kufanya hivyo ni
kuleta mabadiliko kwenye muziki huo ambao soko lake liko juu Ukilinganisha na aina nyingine za muziki.
Msanii huyo alisema kuwa serikali baada ya kuzuia video ya wimbo wake wa Chura imempa Jukumu la kama balozi wa kuelimisha wasanii wenzake ili waache kuandaa nyimbo au kutoa Video zinazokwenda kimyume na maadili.
“Pamoja na wimbo wangu kufungiwa nitahakikisha ninatumia nafasi hii ya ubalozi ili nisaidie Na kuelimisha wasanii wenzangu ili kuandaa kazi zinazolinda maadili yetu,” alisema Snura.
Alisema kuwa serikali imemuona yeye ni mtu sahihi na kumpa jukumu la kuwa balozi wa kuelimisha wasanii wenzake na kuacha kukurupuka kutoa nyimbo bila kuzingatia maadili.

No comments:
Post a Comment